Mfumo wa Kidigitali wa Maoni
Digital Suggestion Box System
📢 e-Maoni
📖 Kuhusu Mfumo wa e-Maoni
Maelezo ya Mfumo
e-Maoni ni mfumo wa kidigitali wa kukusanya maoni, mapendekezo na ushauri kutoka kwa wananchi. Mfumo huu unaruhusu watumiaji kutoa maoni yao kwa urahisi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya QR code na simu za mkononi.
- Kukusanya maoni kwa maandishi na sauti
- Kufuatilia maoni kwa namba ya kipekee
- Taarifa za Vikao na Kuweka Kumbukumbu za Vikao
- Mfumo unawezesha KUjisajili kwenye Vikao kwa kutumia QR-Code
Dira na Dhamira
Dira: Kuwa chombo kikuu cha kukusanya maoni na kuboresha huduma za umma na binafsi nchini Tanzania.
Dhamira: Kuwawezesha wananchi kutoa maoni yao kwa urahisi na kuwawezesha taasisi kuboresha huduma zao kulingana na maoni ya wateja.
- Kuongeza uwazi wa huduma
- Kuboresha mawasiliano
- Kuimarisha uwajibikaji
Jinsi Mfumo Unavyofanya Kazi
Mfumo wa e-Maoni unafanya kazi kwa hatua rahisi zinazomwezesha mtumiaji kutoa maoni yake kwa urahisi na kwa haraka.
- 1. Chanja QR code
- 2. Chagua alama (1-5 nyota)
- 3. Andika au rekodi maoni
- 4. Pata namba ya kufuatilia
- 5. Fuatilia maoni yako
Malengo
Kuboresha huduma za umma na binafsi kwa kukusanya maoni ya wananchi na kuwajibisha taasisi kuboresha huduma zao.
Ubunifu
Kutumia teknolojia ya kisasa kuleta mageuzi katika ukusanyaji wa maoni, kuanzia maandishi hadi sauti kwa urahisi.
Ushirikishwaji
Kuwawezesha wananchi wote bila kujali elimu au uwezo wao wa kiteknolojia kutoa maoni yao na kuboresha huduma.
Manufaa ya Mfumo wa e-Maoni
- Hakuna gharama za ufungaji
- Kuweka Taarifa za Vikao
- Kutumia Mfumo wa QR-Code kujisajili kwenye vikao
- Maoni yanarekodiwa kwa usalama
- Uwezo wa kurekodi sauti
- Namba ya kufuatilia maoni
- Taarifa za wakati halisi
- Rahisi kutumia na simu
- Inaweza kutumika popote
- Inaboresha huduma
⚡ Vipengele vya Mfumo
QR Code
Chanja QR code kwa urahisi ili kutoa maoni yako papo hapo.
Kiwango cha Nyota
Weka alama kwa nyota 1-5 ili kuonyesha kuridhika kwako.
Rekodi Sauti
Toa maoni yako kwa sauti badala ya kuandika.
Fuatilia Maoni
Fuatilia maoni yako kwa kutumia namba ya kufuatilia.
📢 Sauti Yako Inahesabiwa!
Toa maoni, mapendekezo na ushauri wako ili kuboresha huduma za umma na binafsi.